Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi -- ambaye anamwakilisha Rais pia nchini Uswisi, Austria, Poland, Jamhuri ya Cheki, Slovakia, Romania, Bulgaria na Hungary -- aliwasilisha hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa Mh. Rais wa Ujerumani Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin hapo tarehe 06/06/2017.

  • Pichani ni msafara wa Mhe. Balozi mteule Dr. Abdallh Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani akiwasili katika eneo la Ofisi ya Rais wa Ujerumani kwa ajili ya kuwasilisha hati za utambulisho.
  • Pichani ni Mhe. Balozi mteule DR. POSSI akiweka saini katika kitabu Maalumu kabla ya kuwasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Ujerumani.Pichani ni Mhe. Balozi mteule DR. POSSI akiweka saini katika kitabu Maalumu kabla ya kuwasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Ujerumani.
  • Balozi Mteule akiwa mbele ya Gwaride lililoandaliwa maalumu kwa heshima ya Balozi Mteule Dr. Abdallah Saleh Possi kabla ya kukabidhi hati za utambulisho.
  • Mh. Balozi Dr. Abdallah Saleh Possi akikabidhi hati kwa Rais wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier
  • Balozi Dr. Abdallah Saleh Possi akipeana Mkono na Rais wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.