Kwa Watanzania wote

KONGAMANO LA DIASPORA (DIASPORA INVESTMENT CONFERENCE) KUANZIA TAREHE 13 HADI 15 AGOSTI, 2015, DAR ES SALAAM, TANZANIA

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.

Ubalozi unapenda kukufahamisha kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhsirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu zinaandaa Kongamano la Diaspora (Diaspora Investment Conference) Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti, 2015 katika hoteli ya Serena.

Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika nchini Tanzania na litahusisha Diaspora na wadau wa kutokea Tanzania. Aidha, imependekezwa kuwa tarehe 15 Agosti, 2015 Diaspora watafanya ziara Zanzibar kwa mwaliko wa Serikali ya Zanzibar.

Kongamano linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu “Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania” na litajikita katika kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na Kati. Aidha, Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo watapata nafasi ya kunadi fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.

Pamoja na shughuli za ufunguzi na kilele, matukio muhimu yatakuwa ni maonesho ya Kibiashara, Mada na Majadiliano kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.

Taarifa zingine za muhimu zitatumwa kwako siku zijazo.

Imetolewa na:
UBALOZI WA TANZANIA- BERLIN