Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani imemtakia kila la heri balozi wa Tanzania nchini ujerumani anayemaliza muda wake Mhe. Philip Marmo.

 "Tunamtakia kila la heri mheshimiwa Bw.Philip Marmo amekaa na sisi na kutuwakilisha hapa ujerumani si haba" alisema kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki nguli Kamanda Ras Makunja.
Pia alitumia muda huo huo kwa kusema "karibu Ujerumani balozi  Dkt.Abdallah Possi" 

Kamanda Ras Makunja alisema kwa kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda,ni wakati muafaka kwa balozi zetu kuwashirikisha wasanii katika kutangaza soko la Tanzania kimataifa kuvutia wawekezaji na watalii. 

Ngoma Africa band imeitangaza Tanzania zaidi ya miaka ishirini kimataifa na milango ipo wazi kama balozi zitazishirikisha bendi hiyo "tunajua wapi pa kuitangaza na walipo wawekezaji wenye upendo na Tanzania alisema Kamanda Ras Makunja. wasikilize at www.ngoma-africa.com