Kwa Watanzania wote

KUKUSANYA MAONI KWA AJILI YA KUBORESHA MPANGO MAKAKATI WA KUWAWEZESHA VIJANA WENYE VIPAJI MAALUM

Ubalozi umepokea barua ya maombi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya kukusanya maoni ya “Disapora” ili kuandaa Mpango Mkakati wa kuwawezesha vijana wenye vipaji maalum kuwa chachu ya kuchangia maendeleo ya Taifa.

Ubalozi unaomba ufikishe ujumbe huu kwa Watanzania wote waishio Poland ili washiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi hili la kujaza madodoso ya Mkakati huu.

Pamoja na barua hii tunaambatisha madodoso ambayo yanatakiwa kujanzwa na kisha kurejesha Ubalozini ifikapo tarehe 3 July, 2015.

Imetolewa na:
UBALOZI WA TANZANIA- BERLIN